Share

Runinga ya Citizen yarejea chuoni Masai Mara, miezi 3 baada ya #MaraHesit

Share this:

Miezi mitatu baada ya runinga ya Citizen kukuletea makala maalum ya ‘Mara Heist’ ambayo yaliweka wazi njama za wizi wa mali ya umma katika chuo kikuu cha Masai Mara, Wanahabari wetu Asha Mwilu na Waihiga Mwaura wamerejea chuoni humo kufuatilia mambo baada ya ufichuzi huo.
Hii leo saa tatu kwenye taarifa zetu za Newsnight, tutapata kufahamu hatma ya Spencer Sankale na wenzake waliojitokeza kufichua wizi huo. Vile vile utapata kujua jinsia chuo hicho kinavyoendeshwa kwa sasa na pia iwapo kunaye aliyeshtakiwa kutokana na ufichuzi huo.
#MaraHeist

Leave a Comment