Share

Idadi ya juu zaidi ya visa vipya 1,459 vya COVID-19 yaripotiwa Kenya

Share this:

Kenya imethibitisha visa vipya 1,459 vya COVID-19 kutoka kwa sampuli 10,146 zilizopimwa katika muda wa masaa 24 yaliyopita.
Visa hivyo vipya vimeongeza idadi ya maambukizi hadi 74,145, hali ambayo inazidi kuleta wasi wasi kuhusu kiwango cha maambuziki humu nchini.
Kufikia sasa, Wizara ya Afya imefanyia uchunguzi jumla ya sampuli 815,040 tangu kuanza kwa janga hilo.
Kati ya visa hivyo vipya, 1,419 ni vya Wakenya na 40 ni vya raia wa kigeni, kuanzia umri wa miezi mine hadi miaka 97.
835 kati ya waliambukizwa ni wanaume huku 624 wakiwa wanawake.

Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN
Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news
Check our website: https://www.kbc.co.ke/

#KBCchannel1 #KBCNewsHour #KBClive

Leave a Comment