Share

Familia moja Kitengela yalilia haki ya mwana wao

Share this:

Familia moja eneo la Kitengela kaunti ya Machakos inalilia haki baada ya kumpoteza mwana wao wa kiume wiki jana katika hali tatanishi.
Inadaiwa kwamba stephen munga mwenye umri wa miaka 17 alipigwa alipokuwa akihudhuria sherehe katika uwanja wa ngong race course jumamosi ya tarehe 7 mwezi huu hapa nairobi. Kulingana na babake, vurugu lilizuka katika hafla hiyo kufuatia madai ya wizi ambapo mwanawe alivamiwa na kupigwa vibaya. Harakati za kumtafuta katika hospitali na vituo vya polisi zilimuelekeza hadi chumba cha uhifadhi wa maiti cha city siku tano baadaye. Ripoti ya upasuaji ilithibitisha kuwa alipigwa.

Leave a Comment