Share

Baraza la wazee latoa wito wa ukomavu kuhusu ripoti ya BBI

Share this:

Baraza la kitaifa la wazee limetoa wito kwa viongozi kushauriana kwa ukomavu kuhusu mpango wa maridhiano wa BBI. Baraza hilo limesema mchakato wa BBI unafaa kuongozwa na viongozi wote na wala hakuna anayestahili kuachwa nyuma. Likiongozwa na mdhamini wake Kung’u Muigai na mwenyekiti Phares Rutere, baraza hilo ambalo lilikutana na naibu rais William katika makazi yake ya Karen lilihimiza kukomeshwa kwa malumbano kuhusu ripoti ya BBI. Naibu Rais kwa upande wake alitoa wito kwa wazee hao kuwa katika mstari wa mbele katika kuhubiri umoja na kuhimiza siasa zinazoangazia masuala muhimu.

Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN
Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news
Check our website: https://www.kbc.co.ke/

#KBCchannel1 #KBCNewsHour #KBClive

Leave a Comment