Share

Wabunge na maseneta wamepitisha sheria tata za uchaguzi zilizorekebishwa

Share this:

Bunge la kitaifa limepitisha kwa pamoja mabadiliko katika mswada wa sheria za uchaguzi ambao uliwasilishwa pia kwa bunge la senate kupigwa msasa zaidi.

Maseneta aidha wameunga mkono kwa pamoja mswada huo wakitaka kuupitisha haraka tayari kwa kutiwa sahihi. miongoni mwa sheria hizo ni pamoja na ile ya kumtawaza rais mteule iwapo mpinzani wake atajiondoa kwenye kinyang’anyiro.

Haya yamejiri wakati ambapo naibu rais William Ruto amesisitiza kwamba kinara wa Nasa Raila Odinga lazima awe kwenye debe licha ya kutangaza kujiondoa debeni hiyo jana.

Leave a Comment