Share

Vilabu vinavyohangaisha wakaazi kwa kelele mitaani vyaonywa

Share this:

Mamlaka ya uhifadhi wa mazingira nchini NEMA jana usiku ilifanya msako mkali na kuwatia mbaroni wafanyakazi wa vilabu kadhaa jijini Nairobi, ambavyo vilionywa  dhidi ya kuwapigia kelele na kuwasumbua wakaazi wanaoishi karibu na maeneo ya vilabu hivyo vya burudani.
Vilabu vilivyovamiwa ni pamoja B club na Jiweke Tarvern vilivopo hapa jijini Nairobi.
Haya yanajiri baada ya onyo iliyotolewa kufuatia lalama za wakaazi wa maeneo hayo walioiandikia barua mamlaka hiyo wakidai kutopata usingizi kutokana na kelele za vilabu hivyo.

Leave a Comment