Share

Uwajibikaji Kwenye Kaunti : Gavana wa Tana River afika mbele ya seneti

Share this:

Gavana wa kaunti ya Tana River Dhadho Godhana ametakiwa kuandaa upya ripoti za mahesabu ya fedha jinsi zilivyotumika kwenye mwaka wa kifedha wa 2016/2017 na kurejea mbele ya kamati ya seneti kuhusu uhasibu ili kujinusuru kutokana na adhabu kali ya kisheria inayomkodolea macho.
Kamati ya seneti ikiwa ililazimika kukatiza mkao wa leo ambapo ripoti kutoka afisi ya mkaguzi mkuu wa mahesabu iliashiria mianya chungu nzima kwenye makadirio ya kifedha kutoka kaunti hiyo.

Leave a Comment