Share

UTULIVU WAREJEA KIAMAIKO: Makabiliano ya siku mbili yamesitishwa

Share this:

Hali ya taharuki imekua ikitanda kwa siku mbili zilizopita katika eneo la Kiamaiko mtaani Huruma hapa Nairobi, kufuatia kifo cha mwanamume mmoja siku ya Ijumaa wiki uliopita. Mwanamume huyo anadaiwa kufariki katika hali tatanishi huku wenyeji wakidai alipigwa risasi na polisi kimakosa.
Kwa sasa hali ya utulivu imerejea katika eneo hilo huku wapatanishi kutoka dini zote wakifanya mikutano kutafuta mwafaka.
Makabiliano kati ya makundi hayo awali yaliwakosesha wenyeji amani huku yakisababisha uharibifu wa mali, kuchomwa kwa kanisa, magari na kuwaacha wengi na majeraha.

Leave a Comment