Share

Utata wa uopoaji Likoni : Huenda maiti, gari zimeonekana baharini

Share this:

Siku 11 tangu mama Mariam Kighenda na mwanawe Amanda kuzama bahari hindi kwenye kivukio cha Likoni Mombasa, wapiga mbizi leo wametoa habari za afueni wakiashiria kuliona gari walimokuwa wakisafiria wawili hao likiwa mita 58 chini ya bahari hindi.
Wapiga mbizi wa kukodi kutoka Afrika Kusini wakishirikiana na kikosi cha wanamaji nchini walitumia vifaa maalum kuona maeneo ya chini ya bahari huku serikali kupitia msemaji wake Cyrus Oguna ikiashiria kwa asilimia 90 kwamba wana imani gari waliloliona lina miili ya wawili hao.

Leave a Comment