Share

Tume ya kupambana na ufisadi EACC, inajiandaa kwa muamko mpya

Share this:

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini, EACC, inajiandaa kwa muamko mpya ila tu baada ya aliyeteuliwa kuwa afisa mkuu mtendaji, Twalib Mubarak, kuidhinishwa na bunge. Ingawa mabadiliko yanatarajiwa katika jumba la Integrity, tume hiyo bado inakabiliwa na tishio la kuondolewa mamlaka ya kuchunguza ufisadi kupitia mswada ulioko bungeni. Hata hivyo, tume imetetea hatua ilizopiga katika vita dhidi ya ufisadi. Katika miaka sita iliyopita EACC imetangaza mafanikio makubwa katika kuhakikisha wengi wameshtakiwa na baadhi wamerejesha fedha za umma zilizoibwa serikalini.

Leave a Comment