Share

Trela zagongana na mtu mmoja kufariki Sinali

Share this:

Mtu amefariki katika ajali ya barabarani eneo la Sinali huko Voi, leo alfajiri.

Aliyefariki ni dereva wa trela ambaye gari lake liligongana na trela nyengine kwenye barabara hiyo ya kutoka Nairobi kwenda Mombasa. Inasemekana kuwa marehemu alikuwa akisafiri kutoka Mombasa kuelekea Nairobi kabla ya kukumbana na mauti yake. Walisohuhudia wanadai treal hilo lililipuka baada ya ya ajali hiyo na kumteketeza dereva hadi kufa . Dereva wa trela nyingine alinusurika ila anauguzwa katika hospitali ya rufaa ya Voi kutokana na majeraha aliyopata

Leave a Comment