Share

Sherehe ya siku ya wanawake nchini imenoga katika ikulu ya Nairobi

Share this:

Wanawake humu nchini wameungana na wanawake wengine ulimwenguni kuadhimisha siku ya wanawake huku mama wa taifa Bi Margaret Kenyatta akiongoza sherehe hizo katika ikulu ya Nairobi.
Mama wa taifa Margaret Kenyatta ametumia siku hii kuzindua awamu ya pili ya kampeni ya Beyond Zero inayonuiwa kuanza mwaka huu hadi mwaka wa 2022.
Uzinduzi huo unatarajiwa kuambatana na mojawapo ya nguzo nne za serikali ya jubilee ikiwa ni utoaji huduma za afya kwa wote, huku lengo kuu likiwa ni kupunguza kwa kasi idadi ya kinamama wanaopoteza maisha yao au ya watoto wao wanapojifungua.

Leave a Comment