Share

Sakata ya tume ya ardhi : Swazuri na maafisa wengine wakamatwa

Share this:

Aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya ardhi Muhammed Swazuri na wengine kumi ambao wametajwa kuhusika na kashfa ya ufisadi ya ununuzi wa ardhi ya Mombasa Southern by bass watalazimika kukesha kwenye seli ya tume ya kupambana na ufisadi EACC baada ya kukamatwa leo asubuhi .
Swazuri na maafisa wengine ishirini na mmoja wanatuhumiwa kuhusika kwenye ufisadi wa kununulia shamba mamlaka ya barabara kuu nchini, kenha, kutoka kwa kampuni ya Tornado limitted ambayo kulingana na mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji ingegharimu shilingi milioni 34.5 lakini swazuri na wenzake walifanya magendo na kulinunua kwa shilingi milioni 109.7.

Leave a Comment