Share

Sakata ya mahakama: Ujenzi wa mahakama kadha wakwama

Share this:

Idara  ya mahakama JSC hii Jumatano imejipata katika njia panda baada ya kufika mbele ya kamati ya bunge ya hazina na kukosa kuelezea kinaga ubaga jinsi zaidi ya shilingi Billioni sita nukta sita  zilivyotumika kwa miradi ambayo sasa imekwama na hata ujenzi wa miradi hio kusimamishwa.
Kamati hiyo ya hazina  sasa inahofia kwamba huenda wakenya hawatapata huduma bora na pesa zilizotengwa kupotea   kwani hadi kufikia sasa idara ya mahakama haiwezi kuelezea matumizi ya pesa hizo  huku kamati hiyo ikitangaza kuwa itafuatilia  hadi pale pesa hizo zilizofujwa  zitapatikana na wahusika  kukamatwa.

Leave a Comment