Share

Sakata ya dhahabu: Washukiwa 15 kuzuiliwa kwa siku 7

Share this:

Washukiwa kumi na watano ambao walipatikana na dhahabu bandia katika mtaa wa Kileleshwa hapo Jumanne wataendelea kuzuiliwa katika rumande ya polisi ya Kilimani kwa siku saba zaidi   baada ya mahakama kudinda kuwaachilia kwa dhamana.
Aidha, upande wa  mashtaka unasema kuwa kati ya 15 hao, 3 ni raia wa nchi za kigeni na kuitaka mahakama kuwapa siku zaidi kukamilisha uchunguzi kwani magari pia ambayo washukiwa walipatikana nayo ni sharti wayawasilishe kwa mamlaka ya kudhibiti usalama barabarani ntsa kubaini uhalisia wake.

Leave a Comment