Share

Safaricom yawapa usaidizi wanafunzi 100 wa familia maskini

Share this:

Wanafunzi 100 kutoka familia maskini watafaidika na ufadhili wa masomo kutoka kwa kampuni ya Mawasiliano ya Safaricom. Akiongea wakati wa kupokea hundi ya pesa hizo, kaimu waziri wa elimu Amina mohammed, alisema shule zinapaswa kuwa na rasilimali za kutosha kusimamia mahitaji yote ili kuboresha mazingira shuleni. Aidha alisema wanafunzi wote wana haki ya kupewa fursa sawa masomoni. Afisa mkuu wa Maslahi ya Wateja katika Safaricom Sylvia Mulinge, alisema wameandaa miradi zaidi kupitia mpango wa ndoto yetu ili kuhakikisha wanafunzi zaidi wanatimiza ndoto zao.

Leave a Comment