Share

Rais akutana na viongozi wa Jamii ya Abaluhya Ikulu

Share this:

Rais Uhuru Kenyatta amempa makataa ya mwezi mmoja waziri wa kilimo Mwangi Kiunjuri kumkabidhi ripoti kueleza zilivyotumika shilingi bilioni 20 zilizotengewa kufufua sekta ya sukari.
Rais anasema fedha hizo hazikutumika zilivyotakiwa badala yake ziliporwa na matapeli.
Akiongea alipokutana na viongozi kutoka magharibi mwa Kenya katika ikulu ya Nairobi, rais anataka ripoti hiyo pia kutoa mapendekezo jinsi serikali itawasadia wakulima wa miwa.
Kenyatta pia alikutana na viongozi kutoka eneo la Ukambani, wakiongozwa na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka.

Leave a Comment