Share

Rais aidhinisha sheria dhidi ya wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii

Share this:

Ole wako iwapo umekuwa ukiendeleza matamshi ya uchochezi au chuki na kueneza taarifa za uwongo na picha za ngono kwenye mitandao ya kijamii.
Rais Uhuru Kenyatta ametia sahihi sheria ya uhalifu wa mitandaoni ambayo itatumika kwa wale watakaopatikana na makosa ya utumizi mbaya wa mitandao.
Katika sheria hii, hata viongozi wa makundi kwenye mtandao wa Whatsapp almarufu Admin, chuma chao kimotoni iwapo usambazaji na uchapishaji wa taarifa za uwongo na picha za ngono utaendelezwa kwenye Whatsapp, kama anavyotuarifu mwanahabari wetu Daniel Kariuki.

Leave a Comment