Share

Prof. Anyang’ Nyong’o alazwa Aga Khan, Kisumu

Share this:

Gavana na wa Kisumu Anyang’ Nyong’o amelazwa katika hospitali ya Aga Khan baada ya kugua alipokuwa akuhudhuria sherehe za kuidhiinisha askofu wa kaunti ya Kisumu Philip Anyolo wa dini ya kikatoliki.
Kulingana na madaktari wa hospitali  ya Aga Khan, Nyongo’  inasemekana anaendelea kupata nafuu, repoti ya hapo awali ikisemekana kuwa gavana huyo alilazwa  kutokana na kizunguzungu.
Mapema gavana huyo aliwakaribisha naibu wa rais William Ruto na kiongozi wa NASA Raila Odinga baadaye inabainika alitoka kwenye jukwa alipokuwa ameketi akitembea tu kama kawaida ikisemekana na wandani wake alionekana mwenye uchovu asubuhi ya leo.

Leave a Comment