Share

‘’Oyole” hakukaliki!: Maafisa  wawili wa polisi wauawa

Share this:

Hali ya taharuki imetanda eneo la Kayole jijini Nairobi baada ya maafisa wawili wa polisi kupigwa risasi na kuuawa na majambazi usiku wa kuamkia leo.
Polisi hao walikuwa katika maeneo yao ya kazi kabla ya kushambuliwa na kunyanganywa bunduki aina ya Ak47 na simu zao za mkono.
Maafisa wa polisi kwa sasa wamekita kambi mtaani humo hadi kupatikana kwa majambazi hao sugu wanaodaiwa kuwahangaisha wenyeji kwa muda.

Leave a Comment