Share

Onyo kwa kampuni za kamari : Waziri Matiang’i kuwafurusha wamiliki haramu

Share this:

Serikali sasa inalenga kuwachukulia hatua raia wa kigeni waliomo nchini na wanaoendesha biashara ya kamari kinyume na kibali walichopewa na serikali.
Waziri wa usalama wa ndani dakta Fred Matiangi anamtaka katibu wa uhamiaji Gordon Kihalangwa kuanzisha mchakato wa kuwapiga msasa raia wote waliomo nchini na watakaopatika kuwepo kinyume cha sheria warejeshwe makwao.
Alikuwa akizungumza wakati wa mkao na washikadau katika kitengo cha kamari nchini alikoonya kwamba vijana wengi wameachwa hohehahe kutokana na kuhusika kwenyew mchezo huo.

Leave a Comment