Share

Naibu wa rais mteule William Ruto awarai wakenya kudumisha amani

Share this:

Naibu wa Rais William Samoei Ruto  pamoja na mkewe Rachel Ruto   Jumapili walihudhuria  ibaada  katika kanisa la Faith Evangelistic ministries,huku akitoa wito kwa wakenya kuimarisha amani ili  kuwezesha kila mkenya kukidhi mahitaji yake.
 Naibu wa Rais hakusita kukiri kwamba walipata ushindi kwa uwezo wa mwenyezi Mungu na kusisitiza kuwa wao pamoja na upinzani wote ni washindi.
Aliwasihi wakenya kuishi kwa umoja ili kuendeleza  nchi mbele.

Leave a Comment