Share

Naibu Rais William Ruto hatahudhuria mdahalo wa manaibu wa rais Jumatatu

Share this:

Mdahalo wa moja  kwa moja wa wagombezi wa urais na manaibu wao unaonekana unaelekea kutibuka,  huku wagombeaji wakizidi kulalamikia maandalizi duni.
Jumapili kitumbua kimeonekana kuingia mchanga  baada ya Naibu Rais kusisitiza kuwa hatashiriki kwenye mjadala wa Jumatatu, na badala yake atamtuma mbunge wa Kikuyu  Kimani Ichung’wa kumuwakilisha.
Haya yanajiri  huku  wagombeaji sita wa Urais  wakiongozwa na Ekuru Aukot wakitishia kutoshiriki  kwenye mdahalo huo, iwapo kutakuwa na midhalo miwili tofauti mmoja ukimshirikisha rais Uhuru Kenyatta  na Raila Odinga, huku wa pili ukiwashirikisha  wagombea wengine sita.

Leave a Comment