Share

Naibu rais asisitiza kura ya maamuzi ni ndoto ya mchana

Share this:

Kwa mara nyingine tena naibu wa rais William Ruto amesisitiza kwamba juhudi za kubadilisha katiba  kupitia kura ya maoni ili kuunda wadhifa wa waziri mkuu ni ndoto ya mchana akisema haina umuhimu kwa sasa.
Akizungumza katika kaunti ya Uasin Gishu eneo bunge la Moiben wakati alipohudhuria sherehe za kumkaribisha nyumbani katibu katika wizara ya  biashara Chris Kiptoo, Ruto aliwasuta wanaoendeleza ajenda hiyo  akiwataja kama wanaotafuta nyidhifa  kupitia njia ya mkato.

Leave a Comment