Share

Mwenyekiti wa tume ya Ardhi ajitetea dhidi ya shutuma za ufisadi

Share this:

Mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya ardhi Dakta Mohamed Swazuri ameshikilia kwamba taratibu za ununuzi wa ardhi ya ekari kumi na tatu nukta tano eneo la ruaraka hapa Nairobi zilifuatwa, na kwamba hana lolote la kuficha licha ya shinikizo achunguzwe pamoja na makamishna wake.
Swazuri anasema hana lolote la kuficha kuhusiana na ununuzi huo uliogharimu hadi shilingi bilioni moja nukta tano za awali zilizolipwa mmiliki wa ardhi hiyo Francis Mburu.

Leave a Comment