Share

Mtoto mmoja wa Kikei aliyepotea amepatikana

Share this:

Mmoja wa watoto wawili walioripotiwa kutoweka eneo la Thika kaunti ya Kiambu amepatikana hii leo baada ya NTV kuangazia visa hivyo viwili jioni.
Mercy Wagio Karanya alipatikana akirandaranda ovyo ovyo , akiwa ameonekana kuchanganyikiwa. Kwa sasa Mercy mwenye umri wa miaka kumi na miwili yuko katika kituo cha polisi cha Thika alikopelekewa baada ya kupatikana na wasamaria wema. Awali mama yake alikuwa amepiga ripoti katika kituo cha polisi cha Makongeni, Thika, bintiye alikuwa amepotea mtaani Makongeni phase 10. Hata hivyo mtoto mwingine wa kiume Alvin Ngari Kwera mwenye umri wa miaka minne
ambaye vilevile amedaiwa kutekwa nyara katika eneo lilo hilo angali kupatikana. Inadaiwa Alvin alitekwa nyara akiwa na mwanafunzi mwingine wakiwa kanisani siku ya Jumapili . Kijana aliyekuwa ametekwa naye aliachiliwa baada ya siku moja. OCPD wa Thika Paul Kiriki alisema maafisa wa polisi wanachunguza watu kadhaa katika kijiji hicho ili kuwakamata watekaji nyara hao.

Leave a Comment