Share

Minofu hatari : Waziri Cecily Kariuki atoa onyo

Share this:

Watu wawili wameaga dunia katika eneo la Ikolomani kaunti ya Kakamega kwa madai ya kula nyama ya ngombe ,inasemekana kuwa ngombe huyo alikufa lakini wanakijiji hao wakaamua kushabikia mzoga wake.
Kwa hivi sasa watu wengine 19 waliobugia nyama hiyo wanaendelea kupata matibabu katika hospitali kuu ya Kakamega.
Haya yanajiri huku waziri wa afya Cecily Kariuki akionya wakenya dhidi ya kula nyama ambayo haijakaguliwa.

Leave a Comment