Share

Mikakati iliyobuniwa kuwasaidia watoto kutumia likizo kukuza talanta zao

Share this:

Wakati kama huu wa likizo ndefu watoto wengi husalia nyumbani bila kuwa na mengi ya kufanya ila kutazama runinga mchana kutwa huku wengine wakihofiwa kujitosa kwa mambo yasiyofaa. Hata hivyo mikakati mwafaka ikibuniwa ya kuwasaidia watoto kutumia muda wao wa likizo kwa njia inayokubalika kama kukuza talanta zao, hilo ni jambo litakalofana mno. Katika kaunti ya Nyeri, kambi ya usanii iliandaliwa kwa watoto kati ya umri wa miaka 5-15 ambapo walijumuika pamoja na kufunzwa kuhusu usanii kama vile uchoraji na uundaji wa vinyago. Mwanahabari wetu Carol Nderi alikifika kwenye kambi hiyo ya usanii na kutuandalia taarifa ifuatayo.

Watch KTN Live http://www.ktnkenya.tv/live
Watch KTN News http://www.ktnnews.com
Follow us on http://www.twitter.com/ktnkenya
Like us on http://www.facebook.com/ktnkenya

Leave a Comment