Share

Mbunge wa Nyakach matatani: Aduma Owuor akamatwa Kisumu

Share this:

Mbunge wa Nyakach Aduma Owuor amekamatwa mchana wa Alhamisi na maafisa wa tume ya kukabiliana na ufisadi na anapaniwa kusafirishwa hadi hapa jijini Nairobi, kuhusiana na malipo ya hadi shilingi milioni sitini na nane alipohudumu kwenye baraza la jiji la Nairobi kama afisa wa kisheria.
Wakati huo huo afisa mkuu mtendaji katika tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi Twalib Mbarak amedokeza kuwa wameokoa mali ya thamani ya shilingi bilioni mbili nukta saba kwa kutumia njia mbadala katika kipindi cha miezi minne iliyopita.

Leave a Comment