Share

Kizungumkuti cha kamari: Kampuni zilizositishwa bado zinahudumu

Share this:

Juhudi za serikali za kusitisha huduma za michezo ya kamari kwa kampuni 27 bado haijaonekana kuzaa matunda, huku nyingi ya kampuni hizo zikizidi kutoa huduma hizo , nao wacheza kamari wakilalamikia hatua hiyo ya serikali.
Kampuni ya Safaricom, ambayo ni moja ya zile zilitarajiwa  kufunga kabisa nambari ambazo wateja wa kucheza kamari  hutumia kushiriki michezo hiyo , imeitaka bodi ya kudhibiti michezo ya kamari kutoa muda wakutosha kutekeleza agizo hilo ,  kwani baadhi ya wateja bado wana fedha kwenye akaunti zao .

Leave a Comment