Share

Kizungumkuti cha fidia : Familia za walioangamia Ethiopia zalalama

Share this:

Baadhi ya familia zilizowapoteza wapendwa wao kwenye mkasa wa ajali ya ndege ya uhabeshi mwezi uliopita sasa wamelalamikia kuhusu mawakili kutoka nchini Marekani na wa humu nchini ambao wamezidi kuwapigia simu wakitaka kuwasaidia kufuatilia suala la kulipwa fidia.
Kulingana na baadhi ya familia hizo, kampuni ya ndege ya Ethiopia iliahidi kulipa kila familia takriban shilingi Milioni ishirini jambo ambalo limewavutia mawakili mbalimbali wakitaka kuwasimamia kando na mawakili wengine kutoka Marekani wanaowashawishi kushirikiana nao kuishtaki kampuni ya ndege ya Boieng ili kulipwa fidia.

Leave a Comment