Share

Kizazaa kilishuhudiwa katika ofisi za gavana maeneo ya Upperhill

Share this:

Kulikuwa na kizaazaa leo wakati walinzi wa Gavana wa Nairobi Mike Sonko walipokabiliana na maafisa wa kukadiria thamani za ardhi na nyumba katika eneo la Upper Hill.
Gavana Sonko anamiliki ofisi iliyoko kwenye ardhi ya ekari moja katika eneo hilo na maafisa wa EACC wanachunguza ikiwa kiwanja hicho kilinunuliwa kwa njia halali. Imedaiwa kuwa kampuni inayomilikiwa na mkewe ilinunua ardhi hiyo kutoka shirika la reli lakini thamani ya kiwanja hicho inadaiwa kutolingana na thamani yake halisi wakati wa ununuzi. Kwenye purukushani hiyo maafisa wa EACC na polisi walishindfwa kutekeleza uchunguzi wao. Gavana Sonko alikukatika hafla moja na Rais Uhuru Kenyatta wakati vurumae likiendelea upper hill.

Leave a Comment