Share

Kitendawili cha mapacha : Idara ya upelelezi kusaidia kupata uteguzi

Share this:

Angeline Omina, mwanamke anayezingirwa na utata wa kuishi na mmoja wa pacha wa Kakamega waliotenganishwa kwa miaka 19, anasisitiza kuwa mtoto huyo ni wake. Akizungumza katika eneo la Kangemi Omina anasema kwamba iwapo uchunguzi wa DNA utabaini kuwa mtoto huyo sio wake basi itabidi wasimamizi wa hospitali ya Kakamega wampe mtoto wake kwani anauhakika alijifungua. Hayo yamejiri huku makachero wakianza uchunguzi kuhusu sakata ya pacha hao.

Leave a Comment