Share

Kioja cha pacha Kakamega: Mama yao mmoja akamatwa na polisi

Share this:

Siku nne baada ya pacha waliotenganishwa kwa miaka 19 kusisitiza kuwa wameridhika na matokeo ya uchunguzi wa DNA na kuwa hawatashtaki hospitali ya Kakamega, kulitokea na hali ya suitafahamu hapo Alhamisi baada ya Angeline Omina, ambaye alikuwa anaishi na pacha mmoja kutaka kumchukua mwanawe Melvies imbaya kwa  nguvu. Mama huyo alikamatwa na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Kakamega anakozuiliwa.
Mwanahabari wetu Georgina Magondu na maelezo zaidi kuhusu mtafaruku huu.

Leave a Comment