Share

Kioja cha Ikulu : Mwanafunzi wa JKUAT apigwa risasi

Share this:

Jaribio la mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu cha JKUAT kuingia ikulu ya Nairobi huku akiwa amebeba kisu ziliambulia patupu baada ya yeye kupigwa risasi begani na maafisa wa polisi. Brian Kibet anayeuguza jeraha kwenye hospitali kuu ya Kenyatta alipigwa risasi baada ya yeye kupanda kwenye ua la ikulu na kuwatishia maafisa wa polisi kwa kisu. Awali alikuwa amechapisha taarifa kwenye mtandao wake wa Facebook akitishia kuvamia ikulu kwa masaibu anayodai kupitia.
Mwanahabari wetu Kimani Githuku ana maelezo zaidi.

Leave a Comment