Share

Kaunti ya Tharaka Nithi yaathirika zaidi na baa la njaa

Share this:

Kaunti ya Tharaka Nithi ni miongoni mwa kaunti 23 ambazo zinasemekana kuathirika zaidi na baa la njaa nchini. Kulingana na takwimu za Mamlaka ya kukabiliana na njaa nchini, NDMA, asilimia 90 ya mimea katika kaunti hiyo haikuota. Kwa sasa zaidi ya familia 7,000 zinaathirika zaidi suala ambalo limechangia kuwepo kwa ongezeko kubwa la wanafunzi kuacha masomo. Peter Mungai yuko katika kaunti ya Tharaka Nithi ili atujuze zaidi.

Leave a Comment