Share

Jiko la kuchoma taka lazinduliwa hospitalini katika kaunti ya Kwale

Share this:

Jiko la kisasa linalochoma taka za hosipitali ili kuzalisha moto wa kupikia linazinduliwa leo katika hospitali ya Kinondo Kwetu katika Kaunti ya Kwale. Jiko hilo la kijamii ambalo limekarabatiwa na wakfu wa Community Cooker kwa ushirikiano na Planning Systems Services litatumiwa na hospitali hiyo na linatarajiwa kupika zaidi ya vyakula 200 kwa siku kando na kupika vyakula vingine 2500 vya shule ya upili ya kinondo na kuchemsha maji zaidi ya lita 1000. Jiko hilo pia lina uwezo wa kuoka mikate na keki. Madhumuni ya kukarabati jiko hilo ni kutunza mazingira kwa kupunguza ukataji wa miti kwa kuchoma makaa na matumizi ya kuni. Maafisa wa serikali ya kaunti ya Kwale wakiandamana na waakilishi wa wakfu wa Community Cooker tayari wamefika eneo hilo kwa shughuli ya uzinduzi huo.

Leave a Comment