Share

Je wakenya watafahamu ukweli kuhusiana na sakata ya sukari?

Share this:

Madai yameibuka kuwa baadhi ya wabunge huenda walihongwa ili kutupilia mbali ripoti ya kamati ya pamoja iliyokuwa ikichunguza sakata ya sukari ya sumu nchini.
Inadaiwa kuwa pesa kiwango cha hata shillingi elfu kumi zilitamba katika bunge la taifa wakati mjadala huu ulikuwa ukijadiliwa, lengo likiwa kuhakikisha mawaziri watatu wameondolewa lawama ya sukari hiyo kuingizwa nchini.
Haya yanajiri siku chache tu baada ya gazeti la People Daily kufichua jinsi bunge la 12 limezingirwa na ufisadi haswa kupitia kwenye kamati zake.

Leave a Comment