Share

Jaji Sankale Ole Kantai aachiliwa kwa dhamana ya polisi

Share this:

jaji wa mahakama ya rufaa Sankale Ole Kantai ameachiliwa kwa dhamana ya polisi, na kuagizwa kurejea katika makao makuu ya idara ya upelelezi nchini (DCI) kubaini iwapo atafikishwa mahakamani au la kuhusiana na mauaji ya mfanyibiashara wa Kiholanzi Tob Cohen.
Jaji Kantai alisalia kizuizini usiku kucha katika kituo cha polisi cha Muthaiga baada ya kuhojiwa mchana kutwa hapo jana. Makachero waliomhoji leo waliidokezea runinga ya citizen kuwa jaji kantai alikri kufahamiana kwa karibu na sarah wairimu cohen, mjane wa cohen ambaye pia ni mshukiwa mkuu wa mauaji hayo. kantai ameagizwa kurejea katika makao makuu ya dci siku ya jumatatu asubuhi, ili kubaini iwapo atashtakiwa na makosa ya kupanga njama ya kuvuruga uchunguzi wa mauaji ya cohen na kutumia ofisi yake kama jaji kumsaidia wairimu kukwepa mashtaka.

Leave a Comment