Share

Inadaiwa Ksh4m zinazokusanywa za uuzaji wa pombe hazijafika NACADA

Share this:

Uchunguzi umeanzishwa baada ya pesa za leseni za uuzaji wa pombe katika kaunti ya Narok kupotea.

Zaidi ya milioni nne zilizolipwa na wafanyibiashara ili kupata leseni hzaijafikia idara ya kudhibiti matumizi ya pombe na madawa ya kulevya (NACADA). Kamishna wa kaunti ya Narok George Natembeya amethibitisha madai hayo huku akisema afisa mmoja wa kaunti amekuwa akiwalaghai wafanyibiashara na kuwapa leseni ghushi. Kaunti hiyo imeagiza wauzaji wa vileo kuregesha leseni zao ili kubaini uhalali wake. wanadai kuwa afisa huyo amekuwa akipokea kati ya shilingi elfu thelathini na shillingi elfu mia moja na ishirini ili kuwapa leseni.

Leave a Comment