Share

Hospitali ya afya ya mama na mtoto imefunguliwa rasmi Makueni

Share this:

Mke wa rais, Margaret Kenyatta, amefungua rasmi hospitali ya Makueni ya afya ya mama na mtoto.
Hospitali hiyo iliyojengwa kwa muda wa miaka minne na serikali ya kaunti ya Makueni inatarajiwa kuwahudumia zaidi ya watu laki moja. Hospitali ina vitanda 120. Kabla ya ugatuzi kuanzishwa, kaunti ya Makueni ilikuwa na vituo vya afya vitatu vilivyokuwa vikiwahudumia kina mama na watoto, lakini sasa, kaunti imeongeza idadi ya vituo vya kutoa matibabu na kufika kumi na viwili.

Leave a Comment