Share

Hospital mahututi Kerugoya: Inadaiwa wauguzi wameambukizwa Hepatitis A

Share this:

Hospitali ya rufaa ya Kerugoya kaunti ya Kirinyaga haitawalaza wagonjwa isipokuwa tu visa vya dharura kwa muda wa siku 21. Haya ni baadhi tu ya mapendekezo ambayo yametolewa kwenye ripoti ya bodi ya madaktari nchini, kufuatia uchunguzi uliofanywa kuhusiana na mazingira duni katika hospitali hiyo. Ripoti hiyo ambayo imedhihirisha uozo uliokithiri hospitalini humo, pia imependekeza maafisa 6 wakuu wa hospitali hiyo wachukuliwe hatua za kinidhamu na kitaaluma, kutokana na utepetevu wao kazini uliochangia hali hiyo.

Leave a Comment