Share

Hakuna NHIF bila NEMIS! : Magoha aonya wanafunzi wasiosajiliwa

Share this:

Waziri wa elimu Prof. George Magoha sasa amesisitiza kuwa wanafunzi waliosajiliwa katika mfumo wa NEMIS ndio tu watakaopata huduma za serikali.
Magoha anasema mbali na kukabidhiwa vitabu, wanafunzi watakaopokea bima ya afya  ni wale waliosajiliwa pekeee.
Aidha amewaomba walimu wakuu, viongozi wa miungano ya walimu pamoja na tume ya kuajiri walimu kushirikiana pamoja katika azma ya kukuza utekelezwaji wa mtaala mpya.
Magoha anasema masuala yoyote yanayoambatana na utekelezaji wa elimu nchini yanafaa kuangaziwa kwa umakinifu  bila kuzua mijadala isiyojenga.
Haya yakijiri siku moja tu baada ya walimu wakuu wanaokutanika mjini Mombasa kuelezea matumaini makubwa ya wizara kushughulikia changamoto zinaikabili sekta ya elimu.

Leave a Comment