Share

Gavana Sang yuko huru : Aachiliwa kwa dhamana ya SH 500,000

Share this:

Gavana wa Nandi Stephen Sang ameshtakiwa kwa makosa tatu na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tano pesa taslimu na mahakama ya Kisumu.
Sang alifikishwa katika mahakama hiyo baada ya kutiwa mbaroni hapo Jumatatu kwa madai kuwa aliwachochea wananchi kuharibu majani chai katika shamba la Kibwari kaunti hiyo ya Nandi, Sang akidai kuwa ardhi ambako majani hayo yalikuwa yamepandwa, ilikuwa ya umma iliyonyakulikwa kutoka kwa wananchi wamiliki eneo hilo.

Leave a Comment