Share

‘DUNGA UNUSE’ : Eneo mjini Mombasa, lililofahamika kwa mvinyo

Share this:

Je, umeshawahi kuzuru eneo fulani na kitu cha kwanza kinachokuvutia sio watu wake, sio chakula wanachokula au hata maeneo maarufu ya utalii, bali jina la eneo lenyewe?
Haya basi, hii ndio taswira kamili katika kitongoji duni kimoja eneo ya Changamwe, kaunti ya Mombasa ambako husalia kuibua ucheshi na hata maswali mengi kuhusiana na historia yake.
Mwanahabari wetu Shukri Wachu alizuru  eneo la ‘Dunga Unuse’ jina ambalo chimbuko lake ni kutokana na maneno ya jamii ya wataita, “Nkudungie ki” kuashiria kununua mvinyo wa kupimwa ambapo mteja husema, “ndungie nusu” yaani nipe nusu kikombe.

Leave a Comment