Share

BURIANI CHEMJOR: Mwanahabari wa K24 azikwa, Kiboino

Share this:

Mwendazake mwanahabari wa K24 Daniel Chemjor hatimaye amezikwa eneo la Kiboino kaunti ya Baringo.
Chemjor aliaga katika ajali ya barabara wiki mbili zilizopita, baada ya gari lake, kukosa mwelekeo na kutumbukia mtoni.
Wafanyikazi wenza wa K24, jamaa na marafiki, na  wanasiasa, wakiongozwa na Gavana wa Baringo walihudhuria mazishi yake Chemjor, na kumtaja kama mtu aliyependa watu.
Tunamtakia mjane wake jamaa na marafiki faraja, huku tukiendelea kumkumbuka Chemjor kwa mengi kando na kuwa mfanyikazi mwenza alikuwa rafiki wa wengi. Lala salama Chemjor.

Leave a Comment